Fomu Ya Maombi

TARATIBU ZA UPANGISHAJI NYUMBA ZA MAKAZI NA BIASHARA

Tunajenga Taifa Letu
Fomu Ya Maombi
Kurugenzi ya Usimamizi wa Miliki ni moja kati ya Kurugenzi za Shirika la Nyumba la Taifa. Kurugenzi hii inazo idara tatu ambazo zinaendesha shughuli za usimamizi wa miliki nchini. Idara hizo ni,
• Uendeshaji
• Uthamini na Upangishaji
• Uhusiano na Wapangaji

Shughuli zote za usimamizi wa miliki pamoja na zingine kama zilivyoelezwa hapo chini zinafanywa na Kurugenzi hii.

• Kusimamia shughuli za upangishaji wa nyumba za Shirika.

• Kukusanya kodi zote halisi pamoja na malimbikizo.

• Kuzifanyia matengenezo nyumba zinazomilikiwa na Shirika ili kuendana na thamani ya fedha.

• Kuthamini mali za Shirika.

• Kusimamia mahusiano na wapangaji pamoja na kuboresha mazigira ya nyumba za Shirika.

Soma Zaidi

Shirika Kwa sasa linamiliki jumla ya nyumba 16,429. Kati ya hizi nyumba 1,488 ni za wapangaji wanunuzi (tenant purchasers) na wamiliki wa zamani (ex-owners). Nyumba 9590 ni za malazi na 6,839 ni nyumba za biashara. Mpaka sasa Shirika linatoza kodi kiwango cha chini karibu ya asilimia 45-50 ya kiwango cha soko. Hata hivyo Shirika limefanya utafiti wa kodi za soko ambao kwa sasa unalisaidia Shirika kuweza kutoza kodi zake walau karibu na kiwango cha soko kutegemea na eneo la nyumba pamoja na hali ya jengo husika.

Soma Zaidi