DG AWASISITIZIA VIONGOZI WA TAMICO KUWA DARAJA LA MAFANIKIO KWA WAFANYAKAZI

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Bw. Hamad Abdallah, amewataka viongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa TAMICO – Makao Makuu, kuwa daraja imara kati ya wafanyakazi na Menejimenti ya Shirika kwa lengo la kusikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili wafanyakazi ili kuongeza tija na ufanisi.
Bw. Abdallah ameeleza kuwa wajibu wa msingi wa viongozi wa TAMICO ni kuhakikisha kila mfanyakazi anafanya kazi katika mazingira bora, yenye staha na bila changamoto zinazoweza kuathiri utendaji wa kila siku.
“Ninyi ni viongozi wapya mliyochaguliwa kwa imani kubwa ya wenzenu, jukumu lenu ni kuhakikisha mnasemea changamoto zao na kushirikiana na Menejimenti katika kuyapatia ufumbuzi wa kudumu,” alisema Abdallah.
Aidha, Mkurugenzi Mkuu amesisitiza kuwa TAMICO ni kipaza sauti cha wafanyakazi na hivyo viongozi wake hawapaswi kuwa chanzo cha migogoro, bali waendelee kuwa nguzo ya mafanikio, mshikamano na maendeleo ya Shirika. Alibainisha kuwa ofisi yake ipo wazi kutoa ushirikiano pale inapobainika kuna mfanyakazi anayekumbana na changamoto au kunyanyaswa.
Kwa upande wa maslahi ya wafanyakazi, Bw. Abdallah ameweka bayana hatua kubwa zinazochukuliwa na Menejimenti ikiwemo maboresho ya mishahara, kupandishwa madaraja, na maandalizi ya sera mpya ya mikopo ya ujenzi wa nyumba.
“Tutazidi kuboresha maslahi ya wafanyakazi kadri uwezo wa Shirika unavyoongezeka. Hata nyongeza ya mishahara na gawio la Serikali kuongezeka kutoka milioni 800 hadi bilioni 6.5 ni matokeo ya mshikamano na utendaji mzuri wa pamoja,” alisisitiza.
Kwa niaba ya wajumbe, Mwenyekiti wa TAMICO – Makao Makuu, Bw. Agustino Mkate, alimshukuru Mkurugenzi Mkuu kwa kukutana na uongozi na kujadiliana masuala yenye maslahi kwa wafanyakazi. Aliahidi kutoa ushirikiano wa dhati kwa Menejimenti ili kufanikisha malengo ya Shirika.
Kikao hicho kilichofanyika leo ghorofa ya nane, kilikuwa sehemu ya utambulisho wa viongozi wa TAMICO Makao Makuu kwa Mkurugenzi Mkuu, na kimeacha ari mpya ya mshikamano na ufanisi kazini kwa manufaa ya wafanyakazi na Shirika kwa ujumla.
(tarehe 20/08/2025)
JENGO LA NHC NEW BAGAMOYO ROAD LAPATA SURA MPYA BAADA YA KARABATI!

Kamera za NHC zilizokuwapo katika mitaa hiyo zilishuhudia ukarabati huo mkubwa ulioimarisha miundombinu yake sasa inatoa mazingira bora ya biashara na makazi. Wafanyabiashara wana nafasi nzuri za kuendesha shughuli zao kwa ufanisi, huku wakazi wakinufaika na makazi salama, yenye mpangilio mzuri na yanayokidhi viwango vya kisasa.
Mradi huu una faida kubwa kijamii na kiuchumi. Kwanza, unaongeza fursa za ajira kwa vijana na kuimarisha uchumi wa eneo. Pili, eneo limepata mvuto mpya wa uwekezaji, likiwezesha biashara ndogo ndogo na shughuli za kiuchumi kuendelea kwa tija.
Zaidi, maendeleo haya ni ishara ya jinsi miundombinu ya kisasa inaweza kubadilisha sura ya miji mikubwa, kuongeza thamani ya ardhi, na kuunda mazingira endelevu ya kufanyia kazi na kuishi. Plot namba 30A sasa ni mfano wa uwekezaji wa kisasa unaolenga maendeleo ya kijamii, kiuchumi na mijini
(tarehe 01/09/2025)
TAMICO TAIFA YAUMWAGIA SIFA TELE UONGOZI WA NHC

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa TAMICO Taifa, Mhandisi Nchama Wambura wakati akitoa salamu za chama hicho kwenye Mkutano wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa unaofanyika kwa siku mbili tarehe 1 aprili, 2023 na 2 aprili, 2023 , Makao Makuu ya NHC Kambarage House Dar es Salaam.
NAIBU WAZIRI PINDA ATAKA NHC IWE YA KIMATAIFA KWA KUCHUKUA FURSA YA UJENZI WA BALOZI NJE YA NCHI
